"Marriage is our last, best chance to grow up."

Thursday, July 18, 2013

Anaumia Nikigusa

SWALI:
Naomba kuuliza huwa inatokea baada ya kufanya mapenzi na mke wangu hapendi kabisa niguse chuchu zake, hii ni kwa nini?
JIBU:
Asante kwa swali zuri naamini si wewe mwenye kupata tatizo hilo bali naamini ni wanaume wengi hukutana na hili tatizo kutoka kwa wapenzi wao.
Wakati wa kumuandaa kuwa tayari kwa kufanya mapenzi na wakati wa kufanya mapenzi sehemu zinazosisimka hujaa sana damu na kuongezeka size na husisimka sana kuguswa.
Hata hivyo baada ya kufanya mapenzi chuchu zake huhitaji kupumzika hasa baada ya kufika kileleni, hata hivyo baada ya kupumzika hizo chuchu hurudi katika kawaida yake na unaweza kuendelea kuzisherehekea na yeye kufurahia kuguswa.
Unahitaji kumpa muda kidogo chuchu zipumzika baad ya ex ndipo uanze tena.

SWALI:
Hivi kwa nini kuna wanawake wanachuchu kubwa na wengine chuchu ndogo kabisa?
JIBU:
Chuchu ni kama finger prints (alama za vidole) kila mwanamke ana aina yake.
Ingawa wakati mwingine ukubwa wa chuchu huendana na ukubwa wa matiti pia ukubwa wa matiti hutokana na sababu tofauti kama vile kurithi, umri, aina ya vyakula, ujauzito, hedhi na uzito wa mwili.
Kila mwanamke ni tofauti na hii tofauti ipo katika chuchu pia.


SWALI:
Mpenzi wangu ana chuchu zilizogeuka (inverted) hii ina maana gani?
JIBU:
Kwani hujaona watu ambao vitovu (innie and outtie belly button) ni kama vimegeuzwa?
hii ni kawaida na haina tatizo as long as anasisimka na kujisikia vizuri na kwamba wakati wa kunyonyesha mtoto anapata maziwa kama kawaida.
Kugeuka kwa chuchu hakuna uhusiano wowote na kusisimka wakati wa kufanya mapenzi.
Hii ina maana kwamba miili yetu ipo tofauti na wengine.
Muhimu kama zinasisimka, endelea kuzifurahia.


SWALI:
Je ni kweli wanaume huvutiwa na wanawake wenye matiti makubwa?
JIBU:
Ukweli ni kwamba wanaume huvutiwa na matiti.
Hata hivyo ukubwa wa matiti au udogo wa matiti si kiashiria (factor) muhimu ya wanaume kuvutiwa na mwanamke.
Kila mwanaume ana ladha yake, wengine huvutiwa na matiti madogo na wengine huvutiwa na matiti makubwa na wengine matiti si hoja.
Pia inaonesha mwanaume kuvutiwa na matiti ni suala la evolution kwani humkumbusha chakula (kunyonya).
Pia ieleweke kwamba wanaume huvutiwa na mwanamke kwa vipande vipande yaani anaweza kuvutiwa na matiti au midomo au mguu au nywele au matako, shingo au kifua au uso na si matiti pake yake